Mwongozo wa Mbinu Bora katika Kuandaa na Kupitisha Sheria Ndogo za Vijiji Zinazozingatia Jinsia Nchini Tanzania

Toolkit
, 20 pages
PDF (2.07 MB)
21416g-sw.pdf
Language:
English, Swahili
Published: April 2023
Publisher(s):
Area(s):
Product code:21416G

Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka Sheria na kanuni nzuri kuhusu usawa wa kijinsia katika upatikanaji na umiliki wa ardhi, pamoja na uwakilishi katika vyombo vya utawala, sauti za wanawake bado zimekuwa hazijumuishwi vyema katika ugawaji wa ardhi na ufanyaji maamuzi katika ngazi ya kijiji. Kutokana na Sheria za nchi kuzipa serikali za vijiji mamlaka ya kupitisha sheria ndogo ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na asasi nyingine za kiraia Tanzania zimetumia fursa hii kuhamasisha ushirikishwaji bora na wenye tija wa wanawake katika utawala wa ardhi katika ngazi ya kijiji.Mwongozo huu unaelezea hatua kwa hatua namna bora ya kuwezesha jamii katika kuandaa na kupitisha sheria ndogo za vijiji zinazozingatia jinsia nchini Tanzania. Kwa kufanya hivyo, unazipa asasi za kiraia, watetezi na walinzi wa usimamizi wa ardhi na maliasili, wasaidizi wa kisheria na mashirika ya kijamii mchakato unaohusisha wanawake na wanaume katika hatua zote, huku ukitumia mbinu zinazowaruhusu wanawake kuzungumza na kutoa maoni yao.

Cite this publication

TAWLA (2023). Mwongozo wa Mbinu Bora katika Kuandaa na Kupitisha Sheria Ndogo za Vijiji Zinazozingatia Jinsia Nchini Tanzania. TAWLA, Dar Es Salaam.
Available at https://www.iied.org/sw/21416g